Mimi Katikati Poem by Joshua Tesha

Mimi Katikati

Mapenzi ni upeo, mwepesi ka pazia
simaa upatapo, kiagama utanguka
usipitishe mkono, hali kawii funuka
mapenzi maagano, ingawa tupo watatu.

ninani zaidi ya kioo, awezae nichambua
ni baya langu umbo, siri ilo fichika
ni vaapo urembo, nidhamu naishika
mapenzi maagano, ingawa tupo watatu.

nampenda wakidato, ndiye niliye mkolea
kafungwa yake shingo, hajui wangu ubaya
nimemnyima tendo, alisema kalidhika
mapenzi maagano, ingawa tupo watatu.

nilimbusu mikono, mwilini akunishika
akuleta mzozo, nilijua kalidhika
pingu si uzalendo, siri imefichuka
mapenzi maagano, ingawa tupo watatu.

kumbe mimi kajogoo, tetea yupo kimara
uendanaye kariakoo, shopingi yao posta
kafungwa yake shingo, tendo apati kwakea
mapenzi maagano, ingawa tupo watatu.

judi wa makumbusho, ndiko anako lala
nasikia si kwa godoro, chini ndio ujilaza
hakuna apatacho, judi anataka ndoa
mapenzi maagano, ingawa tupo watatu.

mapenzi ni mwanzo, apendaye kwake giza
nivigumu kujua uhongo, utamu rahisi kukolea
sita mmpa kifungo, siri imefichuka
mapenzi maagano, ingawa tupo watatu.

COMMENTS OF THE POEM
READ THIS POEM IN OTHER LANGUAGES
Close
Error Success