Somalia Poem by Abdallah Mpogole

Somalia

Asalam alekumu, enyi wababe wa vita.
Marisau na mabomu, kizazi mwakipukuta.
Mumejaa udhalimu, w wenzenu shingo kukata.
Hamuwezi jitawala, somali zidi umana.

Sad Bare aliingiya, kiasi mliungana.
Koloni la italiya, mkaanza julikana.
Ghafla nyingi Deraya, wenyewe garagazana.
Hakuna wa kwingiliya, Mogadishu chanachana.
Wasomali jirudini, kama kweli muna dini.

Aididi alishika, akombowe Ogadeni.
Wakamwinda Amerika, kawatia adabuni.
Somali aliwashika, kadabisha mashetani.
Wasomali yenu vita, lini amani tafika.

Abisinia kaletwa, amani yenu kulinda.
Si muda akakong'otwa, Al shababi kapanda.
Hawa vijana wa fatwa, mseto ukawashinda.
Somali wendawazimu, handasi zimewapanda.

Lini muache chinjana, Afrika mama acheke.
Mutunze wenu vijana, maadili bora mweke.
Wawe watu wa maana, shuleni muwapeleke.
Somali acha hasama, kwa mola mkatubia.

Umoja wenu ndo njia, asili itapotea.
Kanada mwakimbilia, wabaya wafurahia.
Murudi si asilia, vichwa vya demokrasia.
Wasomali munajua, watoto washapotea?

Kona zote mwazamia, mwajisifu somalia.
Lughayo hispania, Amerika u raia.
Muziki wakuzuzua, quran hujapitia.
Amkeni Somalia, tamaduni sijekufa.

Mwishoni nakwandikiya, Shebe ise kanadiya.
Rudi tuje kwangaliya, ni wapi pa kuanziya.
Asili itapoteya, wasokwao iwe kaya.
Puntilandi acha meli, riziki yake haramu.

COMMENTS OF THE POEM
READ THIS POEM IN OTHER LANGUAGES
Abdallah Mpogole

Abdallah Mpogole

Iringa, Tanzania
Close
Error Success