Vijiti Vyake Poem by Joshua Tesha

Vijiti Vyake

alitikisa matawi mkutimkuti
yakajitega kubwa dogo la mti
eeh wale waliwao si mimi
likapiga ngurumo milimani
mashambani nyumbani limti
awezae ona asemaye sema hivi
walianza alimaliza watoo wote
vimti mizizi shina na matawi..

shida ya shina matawi katikati
paa ukawa mpaka wa shamba ili
mzalendo alikufa ndie mizizi
matawi vipofu vilema viziwi
aliko umia embe ukatika tikiti
mkiki mkiki vidonda majonzi
vimti mizizi shina na mtawi..

alioa apate jamvi likawa zizi
matope yakapanda wakaja inzi
mizizi imekufa vipi shina ustahimili
wazee wabusara tafsirini hili
hamsini ukakopa ukatumia ishilini
kivipi na ulikua na thelathini
shauku ya kuolewa kaoa mzazi
vimti mizizi shina na matawi..

ukienda kwa mke mgeni mlango wazi
ukirudi imefungwa watoto salimini
alikua farida amini na tumaini
umekuta mara tano ujauliza nini
makofi tume zaa hakuna harusi
jogoo wakwetu huwika alfajiri
vimti mizizi shina na matawi.

Wednesday, October 16, 2013
Topic(s) of this poem: social
COMMENTS OF THE POEM
READ THIS POEM IN OTHER LANGUAGES
Close
Error Success