KAPCHANGA MARK KWEMOI

Rookie (22.02.1983 / Kitale, Kenya)

Mazingira Ni Uhai - Poem by KAPCHANGA MARK KWEMOI

Mazingira ni uhai, kila mja aelewe
Hiyo ndiyo yangu rai, kwa siba yangu na wewe
Watu wengi wananchi, hawafaidi wenyewe
Mazingira ni uhai, ni faradhi kuyatunza.

Ukiingia mjini, wapigwa na bumbuazi
Ukiwaona razini, waletaayo machukizi
Razini ja hayawani, hawajali tabia hizi
Mazingira ni uhai, ni faradhi kuyatunza.

Taka zimetapakaa, watu hawawajibiki
Kote zimesambaa, majaa hayatumiki
Mawaidha ‘mekataa, tariki hazipitiki
Mazingira ni uhai, ni faradhi kuyatunza.

Kuenda haja mutoni, ni tabia za wanyama
Nao insi bila soni, huwaauni waama
Kweli tufikirieni, tutunze ‘tu dhima
Mazingira ni uhai, ni faradhi kuyatunza.

‘kata miti kivoloya, ni jambo la kuchusha
Ni moja kati ya haya, ni sharuti kukomesha
Ina faida si moya, kuitunza maisha
Mazingira ni uhai, ni faradhi kuyatunza.

Kutupa taka mutoni, pia huleta balaa
Bila haya wajihini, kana kwamba ni vichaa
Takataka maajini, somba hupata fajaa
Mazingira ni uhai, ni faradhi kuyatunza.

Kiliicho nao mwanzo, hakikosi mwisho wake
Sasa mwaelewa chanzo, mutii msikereke
Mazingara ‘pewe tunzo, mwone umuhimu wake
Mazingira ni uhai, ni faradhi kuyatunza.

Comments about Mazingira Ni Uhai by KAPCHANGA MARK KWEMOI

There is no comment submitted by members..Read this poem in other languages

This poem has not been translated into any other language yet.

I would like to translate this poem »

word flags

What do you think this poem is about?Poem Submitted: Wednesday, April 16, 2008[Report Error]