Nimeuona Mwezi (Mtukufu) Poem by Abdallah Mpogole

Nimeuona Mwezi (Mtukufu)

Rating: 4.0

Nimeuona mwezi jamani,
Nimeuona uking'aa angani..
Si mwezi ule unaodhani..
Ni mwezi bora na usikuwe wa thamani..
Ni mwezi wa kuchuma tulo machungani...

Ni mwezi wa kutoa vilo kibindoni..
Nimeuona mwezi uso na chuki moyoni..
Mwezi bora wa siku thalathini..
Nimeuona mwezi wa watu misikitini..
Nimeuona mwezi wa watu kuuthamini...

Mwezi wa umoja na Amani..
Nimeuona mwezi uso kifani..
Mwezi wa watu kupikika chunguni..
Nimeuona mwezi siamini..
Wasonacho wanasaza na kuweka mikobani...

Nimeuona mwezi naajabia..
Mwezi huu ngependa kwendelea..
Nimeuona mwezi wa sote kwa Mwenyezi kwelekea..
Nimeuona mwezi wa thawabu kujihifadhia..
Mwezi uso na misumari kupigilia...

Nimeuona mwezi maridhia...
Mwezi bora kwa watu kujipatia..
Nimeuona mwezi labda kufuzu tutafikia..
Nimeuona mwezi nawe uje kwangalia..
Bora katika miezi, Ramadhan nakwambia...

COMMENTS OF THE POEM
READ THIS POEM IN OTHER LANGUAGES
Abdallah Mpogole

Abdallah Mpogole

Iringa, Tanzania
Close
Error Success