KAPCHANGA MARK KWEMOI

Rookie (22.02.1983 / Kitale, Kenya)

Penye Nia Ipo Njia - Poem by KAPCHANGA MARK KWEMOI

Hebu leo nikweleze, ewe wangu mwandani
Akilini silibanze, ulifikiri undani
Shetani sikufyonze, uwe wangu mkinzani
Usije kulia ngano, ikakutoa peponi.

Penye nia pana njia, maanani tilia
Bila moyo kuhofia, bidii we tilia
Si akili kulalia, pasi kuitumia
Usije mbuzi kuchinja, kwa akili ya kinofu.

Ukembeo siujali, jali yako lisani
Kwanindo yako mali, tapokea kwa hisani
Lugha yako ya kujali, vipi witupe kwani?
Jihadhari wangu mwenzi, ulimi sije kufunga.

Sipendi ukose hali, uanze nichukia
Ukiwa mwenye akili, chunga zako hisia
Upime yako ratili, ndipo upate amua
Hata senti sije kosa, ya mkunguni kusagia.

Mayahe wasosoma, wazunguka mitaani
Wamrisha simama, na kucheki mikobani
Sithubutu ita mama, tajikuta shidani
Kwa kweli namna huna, ni wajibu jiepushe.

Sioni choyo mwandani, wasia kukupa wewe
Fungua moyo mwandani, uchukue mwenyewe
Sivyo nilivyokudhani, kuwa bwege ndiye wewe
Kwa hiyo huu ndo mwanzo, wala sio mwishowe.

Beti saba kamili, kila la kheri mwenzi
Dhiki stahimili, tulienzi letu penzi
Sijibu ukatili, yameniishia machozi
Kumbuka bahari pana, ni kirefu kina chake.


Comments about Penye Nia Ipo Njia by KAPCHANGA MARK KWEMOI

  • (6/22/2009 6:35:00 AM)


    I love your poems.Particularly this, I read it every time a get a chance and it surely leaves me a better person.Thank you KWEMOI (Report) Reply

    0 person liked.
    0 person did not like.
Read all 1 comments »Read this poem in other languages

This poem has not been translated into any other language yet.

I would like to translate this poem »

word flags

What do you think this poem is about?Poem Submitted: Wednesday, April 16, 2008[Report Error]