ukubwa umbali wake
salama kiko mbali
napenda mlango wake
umegeukia mashariki
ndivyo walivyo wazee
hupenda kutenda haki
yamkini wangejua
bora kiwe mbali
kimezingilwa na mitete
uzio wake vimti
jua upitisha miale
mlango wake niwazi
sauti za wanawake
unikatisha kazi
yamkini wangejua
bora kiwe karibu
asubuhi nala mikate
jioni wali samaki
naziepuka kande
tabu hazizoeleki
najibana hata itokee
usiku mimi sitoki
yamkini wangujua
bora kiwe karibu
furaha kwenye sherehe
ukiendesha hawasikii
akija yule mzee
aendaye hato riziki
huto sikia kelele
basi huko hakutoshiki
yamkini wangejua
bora kiwe karibu
This poem has not been translated into any other language yet.
I would like to translate this poem