Wamoyo (Swahili Language) Poem by Grace Pantaleo

Wamoyo (Swahili Language)

Kutwa, kucha nakuwaza,
japo wewe wanikwaza,
wafanya moyo wangu kudunda,
hata nikachukia kitanda.

Acha kunipa mawazo,
nahitaji lako tulizo,
usibwage wangu moyo,
nikakimbia zangu nyayo.

Fanya hima sichelee,
nijihisi wa pekee,
mwili wangu unenepe,
niachane na mapepe.

Wamoyo wangu Wamoyo,
tupilia mbali choyo,
karibu nami sogea,
nipate cha kuongea.

Wajua tunapendeza,
sina haja kujikweza,
usicheze nami mbali,
punguza yako makali.

COMMENTS OF THE POEM
Jacob 13 November 2019

Lovely and nice poem keep it up

0 0 Reply
Ferdinand Maniraguha 23 December 2015

hhhhhh kumbe shairi kama hili, latoka wapi bila wewe Grace, kazi nzuri kweli

0 0 Reply
Dickson Mseti 18 March 2012

mahabuba wa moyo uliyemthamini kwa lugha yako mwanana.endelea kuandika dada.

0 0 Reply
READ THIS POEM IN OTHER LANGUAGES
Close
Error Success