Kijana lako sikio, nataka usikie,
Kimya kujiri, kutamba nataka,
Maanani tieni, nataka fahamu,
Vipi, nikupende?
Vioni ‘tazameni, msije danganywa,
Tumbuizo sikieni, msije’fa bila kuonja,
Tingisheni viuno, japo itafika ufe,
Vipi, nikupende?
Kiumbe natamba, si ngano za kizazi,
Nyimbo naimba, si za utamaduni,
Vicheko kujiri, mkibeza wenzenu,
Vipi, nikupende?
Tamati nafika, kufilisika kwa maneno,
Singependa kutua, yangu kalamu,
Ahadi ya mauko, inanitia wasiwasi kuitua,
Vipi, nikupende?
This poem has not been translated into any other language yet.
I would like to translate this poem