Members Who Read Most Number Of Poems

Live Scores

Click here to see the rest of the list

(30, July 1982 / Iringa, Tanzania)

What do you think this poem is about?

For Example: love, art, fashion, friendship and etc.

Thamaniye Chupi

Wapo watu na porojo, chupi kutoithamini.
Nalileta kwenu zogo, nijibuni niamini.
chupi thamaniye togo, na ereni sikioni?
Thamani utaijua, siketi wakiivua.

Mwingine alinambia, havai kiso maana.
Akivaa sintojua, Pamoja tutafanana.
Hadhi ya chupi najua, ndo hasa ninapingana.
Thamani utaijua, suruali ikichanwa.

Swali langu la kijinga, majibu mazuri nipe.
Kwa msuli kujifunga, chupi haiwekwi pweke.
Hata wavaao kanga, paso chupi sekeseke.
Thamani utaijua, pale kanga ikilowa.

Tamati nasisitiza, chupi thamaniye kubwa.
Uliza wanolegeza, makalio yanazibwa.
Chupi si ya kubeza, si mtoto si mkubwa.
Thamani utaijua, nguo zote zikiibwa.

Submitted: Tuesday, July 09, 2013
Edited: Saturday, July 13, 2013


Read this poem in other languages

This poem has not been translated into any other language yet.

I would like to translate this poem »

word flags

What do you think this poem is about?

Poet's Notes about The Poem

Imefikia msemo miongoni mwa watu ati kwamba chupi kazi yake ni nini, mtu akivaa haionekani au asipovaa pia haionekani, hivyo basi nikaona ni bora niwajuze/ tujuzane na watu wengine kwa kile mie ninachoelewa juu ya thamani ya chupi kama vazi.

Comments about this poem (Living In by Abdallah Mpogole )

Enter the verification code :

There is no comment submitted by members..
[Hata Bildir]