Ikulu ni jumba gani? Mbona watu waliota!
Heshima na kitu gani, watu huenda kufata.
Mbio lukuki za nini, kisa mpana ukuta?
Kipi hasa chawavuta, kuitwa jina Rais?
Kikosi hakipanguki, toka enzi ya Hayati.
Vikongwe hawabanduki, wanavutana mashati.
Vijembe vita na chuki, makundi na mikakati.
Ipo biashara gani, Mwalimu aliuliza.
This poem has not been translated into any other language yet.
I would like to translate this poem