Maishani ubora wa umri kwenda,
kila dakika inayosonga yazidishe mawanda,
Dunia ya leo vyema jitafutie kitanda,
heshima taipata na wasokwao taja walinda,
Umri kwenda busara muda muafaka kujiwinda,
Angaza kijipinda uwatafutie makinda,
Si kuokoteza kona zote hakika yataja kukushinda,
mbegu bora hebu panda iweze zaa mema matunda,
Mola mwombe akubarikie na shukrani iso ya punda,
mieziye kadha taja vuna kile bora lichopanda,
Siishie kuyumba na kelele kama debe shinda,
Uongoke kwa matendoyo katu sijechupia kuangukako,
furaha ya kuzaliwa ni tunu na kuzaa kungalipo.
This poem has not been translated into any other language yet.
I would like to translate this poem