Hatima Poem by Joshua Tesha

Hatima

Nivigumu kumeza
yapitayo kooni mwangu
nimaumivu mazito
yachosha kifua changu
eeh mora nisaidie
nisahau msiba na wake uchungu

mimi sikitu bure
maisha toba yangu
furaha huzuni yangu
umaskini ukaniponza
liziki imenipa uwepo
na yadhati mapenzi yametoweka

ni faida ya wafitini
kula sahani yangu
yao ya akilini
nikawaza yupi ndugu nami
leo kaniibia
kesho yu nyumbani kwangu
eeh mora nisaidie
nisahau misiba nawake uchungu

yeye si yupo nami
kanichoma mkuki shingoni
damu yake ya kwangu
leo kanipa ya shetani
nipite uende uendako
usiage tena usirudi
liziki imenipa uwepo
na yadhati mapenzi yametoweka

kila siku upo kwangu
ndugu yako shoga yako
yamkini umnafiki wewe
ujapo uja na umbea wako
eeh mora nisaidie
nisahau msiba nawake uchungu

sibora unge mfariji
liziki yako angekumbuka
leo kajaa upepo
mimi sili wala silali
miaka sija mwona
hanitamani hanipendi
liziki imenipa uwepo
na yadhati mapenzi yametoweka.

Wednesday, October 9, 2013
Topic(s) of this poem: LOVE
COMMENTS OF THE POEM
READ THIS POEM IN OTHER LANGUAGES
Close
Error Success