Marbet Daniel

Rookie - 89 Points (Kenya)

Mwamko Mpya - Poem by Marbet Daniel

Hongera kwa wanakenya, kwa amani kudumisha
Uchaguzi tumefanya, na katiba kupitisha
Uamuzitumefanya, sote kutuunganisha
Asubui njema Kenya, twang'oa nanga upya.

Makasisi kanisani, mzidi kutufunzeni
Bado twawatazameni, twaskiza kwa makini
Sisi wale wahumini, mabaya tutatendani?
Asubui njema Kenya, twang'oa nanga upya.

Wasiasa fikirini, mkomeshe ubishani
Sisi twawatazameni, twawadai tulipeni
Ahadi sasa ni deni, yaliyo yetu lipeni
Asubui njema Kenya, twang'oa nanga upya.

Vijana mjitoeni, inchi yetu jengeni
Uongozi chukueni, utandawazi tumieni
Toeni nchi chini, mfikishe kileleni
Asubui njema Kenya, twang'oa nanga upya.

Matumaini tunayo, zuri katiba tunayo
Amani twapata kwayo, usawa pia ni kwayo
Ikosayo ni kiliyo, kwayo twasema ndiyo
Asubui njema Kenya, twang'oa nanga upya.

Uaminifu kushika, kwa vita kukomesheni
Bila ya silaha kushika, tu pamoja kazini
Ruwaza tatimizika, lifu mbili thelathini,
Asubui njema Kenya, twang'oa nanga upya.

Shukurani ni kwa mola, bilaye tusingeweza
Kuuandika nakala, kwake katoka uweza
Uzuri yake naila, utamuyie yaliwaza
Asubui njema Kenya, twang'oa nanga upya.

Comments about Mwamko Mpya by Marbet Daniel

There is no comment submitted by members..Read this poem in other languages

This poem has not been translated into any other language yet.

I would like to translate this poem »

word flags

What do you think this poem is about?Poem Submitted: Thursday, February 14, 2013[Report Error]