Nchi yetu Kenya ni rembo, tuipake mafuta
Tuishi kama kitambo, kusiwe navyo vita
Nipende kwa kila jambo, sisi wote twapita
Tumwache hajambo, tusije baki kujuta
Kupokea namba wani, kuishi si kukura
Uraia kweli deni, kulipa nako bora
Tuwe bara au pwani, ni kwazo zetu sera
Twelewe kulikoni, amani kwazo kura
Uraia kufaana, kwa shida na raha
Haja gani kupigana, kinyama bila siha
Twajibike Kenya bana, kwelewa uraia
Nayo mambo yakibanana, upesi kuyatwaa
Tupunguzeni lawama, jamani sijivune
Twataka u usalama, jirani sipigane
Upenda kuutazama, shida tuzikane
Tuutende huu wema, mabaya tuyakane
Uraia si ulafi, ni kupinga utani
Wasilete mali ghafi, kututia unyani
Viongozi ni wasafi, wanaoleta fani
Hatutaki ukorofi, huharibu amani
Mama zetu boresheni, ukulima na hali
Utu nao tufunzeni, tuwe walo tuli
Sote tutafurahini, raia mkijali
Uchumi imarisheni, tupate nazo mali
Watoto tusichoshwe, matusi au ghasia
Twakana tusipotoshwe, mawaidha pasia
Kwa matendo twelimishwe, na tupewe husia
Uraia tuonyeshwe, uje kama masia
Namaliza langu somo, shairi la shauri
Maovuni hapa simo, twabiri lipi gari
Jiulize yaliyomo, kubadili safari
Nafika kwa hiki kikomo, kuomba la kadiri
This poem has not been translated into any other language yet.
I would like to translate this poem