Ndoano Tupu Poem by Dotto Rangimoto

Ndoano Tupu

Dotto naja na maneno, naomba kuwapatia,
Si mengine ni hayano, nudhumu nilotungia,
Msinigune mguno, yakiwa sio sawia,

Jini hupatiwa chano, wenzangu nawaambia,
Chenye mbuzi au funo, na nyudi za kunukia
Hapewi li tupu neno, halafu akatulia,

Pasi na chambo ndoano, jama haijatimia,
Shuti itiwe vinono, venye tamaa kutia,
Ndipo atanasa pono, asiweze kukimbia.

Sasa niwape mfano, upate kuwaingia,
Uliotupu mkono, kitu usoshikilia,
U sawa na kisigino, ambacho twakanyagia.

Zinatosha beti tano, zikikithiri udhia,
Sitaki kunena mno, hapa kikomo natia,
Tangu hapo sina wino, mana umeniishia.

MSAMIATI
Funo.....mnyama jamii ya paa
Pono....aina ya samaki

03 January 2019 Alhamis 13: 00
Jina la Mtunzi Dotto Rangimoto.
Jina la Utunzi Jini Kinyonga
Simu +255762845394 Morogoro.

Ndoano Tupu
Sunday, January 6, 2019
Topic(s) of this poem: january
COMMENTS OF THE POEM
Sofia Kitwana 12 January 2019

asante kwa utenzi wa lugha yetu

1 0 Reply
READ THIS POEM IN OTHER LANGUAGES
Dotto Rangimoto

Dotto Rangimoto

Morogoro
Close
Error Success