Uraia Poem by priscah Mutswenje

Uraia

Pwani kote hata bara, kasikazini hatutakuwa
Tupange manufaa sera, kutufaa kila mara
Uraia bora ni kura, kusiwepo na kukara

Utu tajika twautaka, utu lazima tauweka
Ukweli napo kuushika, Amani tajika tashuka
Wema milele kitukuka, siasa nasi tapendeka
Kura zetu siposafika, dawama sisi tahangaika

Sote pamoja tuwajibike, kura twende twandikishe
Nia zetu zieleweke, mapana marefu twakikishe
Jamaa hakika tusichoke, wasofaa wakuu badilishe
Tuloomba lifanyike, wakuu walobobea tupitishe

Tupunguze tumbi lawama, uamuzi wetu kuchunga
Kupata tosha usalama, tangamano budi kutunga
Katibetu kuitazama, shida twanze kuzipanga
Uchaguzi ‘wo ulo wema, mabaya yano kuyachonga

Twomboleza kila mwaka, Wakenya kufata chama
Kuzikwa kwa kuu chaka, kwo tuvito visivyo wema
Viongozi wanyoofu saka, mufti njia bora kupima
Twondoke la simba chaka, kura siuze kwa Mama pima


Kupiga kura si ombi haki, wananchi njoo twendeni
Kuchagua kwa halaiki, siwe chai na kampeni
Tuweze kuhakiki, wachapakazi juu chini
Meya mbunge Mstahiki, chagua upesi jamani

Tuwe macho wananchi, nchi kamwe tusishtumu
Misafara kwenye nchi, silete kwety hukumu
Chagua kutazama mechi, maisha yawe magumu
Lakini kujitoa panchi, maendeleo yatadumu

COMMENTS OF THE POEM
READ THIS POEM IN OTHER LANGUAGES
Close
Error Success