Urembo Ni Hulka, Sura Ni Sanamu Poem by Hesbon Nyamweya

Urembo Ni Hulka, Sura Ni Sanamu

Anayenipenda leo, kesho siwezi dhamini.
Naweza kuwa Romeo, nife bilayo imani.
Vitendo kama video, mie siwezi dhamini.
Nisije kawa mumeo, hatima niumie moyoni.
Urembo ni hulka, sura ni sanamu.

Mapenzi ni kama karata, kupata na kupotea.....
Ulimbwende sifuata, ndanimo imeozea.....
Hata mwendo kama bata, sitamani si'rekea....
Mwiliyo sije kunguta, ukahaba kabobea....
Urembo ni hulka, sura ni sanamu.

Wa kupenda ni wengi, wa kuishi ni nadra....
Ndoa hufanywa mingi, ila huishia talaka....
Maanani kwa rangi, usitilie mafuta....
Siri ni kama mtungi, ukijua tachizika....
Urembo ni hulka, sura ni sanamu.

Chemacho chajiuza, kibaya chajitembeza.....
Ujuzi kwake ajuza, sikose kuwauliza.....
Usiishipo kwa giza, ukaja kujipumbaza.....
Mapenzi ni kuyakuza, sivyo utajiumiza....
Urembo ni hulka, sura ni sanamu.END

Thursday, December 7, 2017
Topic(s) of this poem: love
COMMENTS OF THE POEM
READ THIS POEM IN OTHER LANGUAGES
Close
Error Success