Anayenipenda leo, kesho siwezi dhamini.
Naweza kuwa Romeo, nife bilayo imani.
Vitendo kama video, mie siwezi dhamini.
Nisije kawa mumeo, hatima niumie moyoni.
Urembo ni hulka, sura ni saamu.
Mapenzi kama karata, kupata na kupotea.
Ulimbwende siyafuata, ndanimo imeozea.
Hata mwendo kama wa bata, sitamani si'rekea.
Mwiliye sije kunguta, ukahaba kabobea.
Urembo ni hulka, sura ni sanamu.
Wa kupenda ni wengi, wa kuishi ni nadra.
Ndoa hufanya mingi, ila huishi talaka.
Maanani kwa rangi, usitilie kwani ni mafuta.
Siri kama mtungi, ukiyajua utachizika.
Urembo ni hulka, sura ni sanamu.
Chemacho chajiuza, kibaya chajitembeza.
Ujuzi kwake ajuza, sikose kuwauliza.
Usiishipo kwa giza, ukaja kajipumbaza.
Mapenzi ni kuyakuza, sivyo utajiumiza.
Urembo ni hulka, sura ni sanamu.
This poem has not been translated into any other language yet.
I would like to translate this poem
Nice piece. I enjoyed reading.
thanks dear i appreciate