Daktari alisema kula tufaha ni afya
Tufaha ni tamu na tena ni kinga
Ukila magonjwa yakuondokea.
Nimekula tufaha si mara moja.
Daktari alisema halina kiwango
Lakini nimekula tufaha lililokuwa na mdudu
Tumbo langu limepata uvimbe
Daktari anasema mdudu hana madhara.
Daktari amenichanganya
Tumbo limezidi kupata uvimbe
Amesema dawa ni kuendelea kula tufaha
Mdudu utakuwa tumboni miezi tisa.
Kweli tufaha halina madhara
Uvimbe sina tena
Shukrani kwake Mungu
Kazi kwangu ya kumlea mwana.
Kweli tufaha ni tunda!
I request the author to kindly translate the poem for the benefit of the readers/ visitors of poemhunter.com
This poem has not been translated into any other language yet.
I would like to translate this poem
Insha njema. The symbolism is amazing and really well thought off.
Thanks Charles