Kerra Poem by priscah Mutswenje

Kerra

Bora zetu barabara, kwa ubora usafiri
Mefungua hata Bara, kuwezesha waabiri
Ni fanisi hii sera, kuwafaa wasafiri
Kwetu vikuu vipera, KERRA inayo hiari

Meinua asilani, uchumi kupanda ngazi
Viungani vijijini, , mewezesha wakazi
Sijizike pilikani, kutatisika kikazi
Heri ipo mashinani KERRA kwayo kazi

Heko kwako KERRA, kuwafaa wachochole
Hali duni ilokera, kutuweka vyovipele
Uchumi ulodorora, sasa metweka kilele
Tusherehekee sera, shangwe na vigelegele

Mashamba mumeboresha, ni KERRA mwezesha
Kibali chayo Maisha, bora ngao kutituvisha
Urembo kuzidisha, mabonde kuhairisha
Minyororo kuondosha, uchumi kupandisha

Lami nazo metandika, kokoto kulainika
Ajira'tu kuinuka, na waja kubamika
Mauzo yameboreka, vijiji ndo kusifika
Adamu kumakinika, siwe baki kunyongeka

Na nauli kulipika, mashinani ni furaha
Kwa miaka na mikaka, ilibaki tu buraha
Wakenya tulisongeka, shabiki wenye karaha
Puani zikatutoka, vijijini patashika

Sasa raha starehe, gari zetu kuendesha
Usukani kama shehe, ustahdi poromosha
Umeondoa kiwewe, hasara kuiondosha
KERRA utu ni wewe, metufaa kimaisha

Pongezi kwako KARRA, kutujali mashambani
Zetu hali kawa bora, shughuli zatu laini
Twekeze bila kupora, za watokao mijini
Na viwanda vyenye sera, kusimama mashinani.

COMMENTS OF THE POEM
READ THIS POEM IN OTHER LANGUAGES
Close
Error Success