Kiswahili Weye Wangu Poem by Abdallah Mpogole

Kiswahili Weye Wangu

Ikiwa Kiswahili ni Mzazi wangu hakika sintokutupa'

Ikiwa ni wewe mlezi, ni vipi mie nikakutupa!

Ukubwa wa umbo langu si hoja, sijaweza hata kuchupa!

Kiswahili uwe wangu, naahidi kuongeza mapendo katu hutogonjeka'

Nitakulisha kama ulivyonilisha na sintachelea ukapunjika'

Nimeona majirani wakivisha zao, zilo na simanzi ati zimeanza cheka'

Kwanini sie mie kwa changu kiswahili, ewe Mama Afrika'

Ninayo mengi ya kusema, kwa machache nadhani ujumbe utafika'

'Kidumu Kiswahili'

COMMENTS OF THE POEM
READ THIS POEM IN OTHER LANGUAGES
Abdallah Mpogole

Abdallah Mpogole

Iringa, Tanzania
Close
Error Success