Mfuko Huu Poem by priscah Mutswenje

Mfuko Huu

Mfuko huu wafaao, ya uzee hifadhi
Tumepata manufaa, bengi hii ya hadhi
Baadaye ukijaa, taona yake radhi
Tatwaa ushujaa, soteni ustadhi

Metufunza kuu somo, NSSF tegemeo
Metuvaa kwenye shimo, kutuzimia mlio
Liojaa milalamo, katu sio upeo
NSSF kuu kimo, kutupa ufunguo

Mwafaka huu mpango, kuelekeza vihela
Umetutoa matongo, yalotutia jela
Asa mefungua bongo, kuweka mijihela
Tuliishi kwa uongo, kutoweka kwa ghala

Na nilivuja awali, sasemi nahifadhi
Niliishi kidalali, asokuwa na radhi
Kachagua yu Jalali, kuporomosha kadhi
Ujumbe ulo halali, unoleta mawaidhi

Miaka nne mepita, kiangaza ya mbele
Kibaba ndi siposita, walisema ya mbele
Punde chururu kipata, tafikiya kilele
Kwaheri kwa yalipita, sitokiri kwa mwele

Miradi takamilisha, japo ya uzeeni
Uchumi kuupandisha, kwa yetu magaleni
Hali i kutoishusha, kwino yenu kampeni
Maisha kuyadumisha, shidani tokomeni

Afari tuliokenda, ya mbali si karibu
Na mali tilioponda, hakika sihesabu
Ingawa tuliipenda, twagundua sulubu
Na yote tuloyapenda, yangetia aibu

Ange sasa titaketi, kusubiri karamu
Bora tupo masharti, tulelewe yatodumu
Ametupa vino viti, kumbi tusikimu
Amezikata tikiti, starehe kukirimu.

COMMENTS OF THE POEM
READ THIS POEM IN OTHER LANGUAGES
Close
Error Success