Nduguyo Poem by Abdallah Mpogole

Nduguyo

Ukijua jambo jema unijuze ndugu yako...

La kututia nguvu mwili sinifiche ndugu yako...

Kama ni ilmu ya manufaa unifunze ndugu yako...


Sinitenge kwa ulacho hata kidogo sinifishe njaa ndugu yako...

ufanye kwangu na mie nifanye hayo kwako...

Kwa uzima na umauti mie ntakuwa ndugu yako...


Litokealo kwa uwezo wake mola, sie tuwe wastahimilivu...

Nimekukumbuka ndugu yangu, apendapo yeye twaja kuonana tena...

Amani, upendo na utulivu vitawale maisha yako...

COMMENTS OF THE POEM
READ THIS POEM IN OTHER LANGUAGES
Abdallah Mpogole

Abdallah Mpogole

Iringa, Tanzania
Close
Error Success