Sikuipenda dunia niliyoishi,
Na sikupenda vile nilivyoishi.
Dunia ilo na Jua na kila aina ya nuksi,
Watu waso na kauli, Vinywani mwao matusi.
Hakika Siamini kama naweza endelea kuishi.
Nimeishi sana nimechoka,
Natamani muda huu kuondoka.
Niende mbali kule nisikofika,
palo ugumu kushika na paso sikika.
Utanikosa japo mawazoni sintokutoka,
Usisononeke na iwapo wantaka,
Jitahidi kulala na ipo siku njozini utaniota.
This poem has not been translated into any other language yet.
I would like to translate this poem