Shairi: Nzi wastaarabu.
Mtunzi: Josiah M. Rodgers.
Umewaona wale nzi wastaarabu,
Wanazunguka kote bila aibu,
Wamejibandika jina nyuki,
Wamejitia bandia mikuki.
Umewasikia wale nzi wastaarabu,
Wanavuma wakiukana ububu,
Wana asali midomoni,
Lakini damu mikononi.
Hujawaona kwenye sahani,
Chunga usiwatie mdomoni,
Shida watakusababishia,
Tumbo lako utalichukia.
Nzi wastaarabu kwenye mchuzi wameingia,
Wananchi midomoni tumewatia,
Shida tumboni tumejiletea,
Hela za nchi zote wameotea.
Mwananchi bado wadhani wale ni nyuki,
Hujawaona wameleta ufisadi na chuki,
Watakunyonya hao ni nzi wastaarabu,
Chungana nao usipate taabu.
Wewe nzi mstaarabu siku zako saba zaisha hivi karibuni!
By Josiah M. Rodgers.
This poem has not been translated into any other language yet.
I would like to translate this poem
this is a great shairi, i love the style and delivery. feel free to review my shairi on spikespoetry.blogspot.com