Jua huipenyeza nuru,
Nuru njema ya asubuhi,
Hupenya ndani ya moyo wangu,
Kuamsha matumaini,
Na hisia mpya.
Moyoni yupo mtu mmoja,
Wa pekee,
Asiye nacho kifani,
Kwa maisha yangu yote,
Humu duniani.
Kwa sababu,
Umeamsha hisia mpya,
Hisia ziujazazo moyo wangu,
Kunipa mawazo,
Huku nikiwa na faraja.
Nimeamini tangu siku ile,
Ya kwanza tulipokutana,
Kuwa kwa hakika,
Utakuwa wangu,
Kwa sababu,
Unastahili hivyo.
This poem has not been translated into any other language yet.
I would like to translate this poem
What does it mean in english?