Chanda chema huvikwa Pete,
Moyoni ushanitia mkanda,
Hadi nchi ya ahadi,
Nachovya asali kwa maziwa,
Penzi lako ni kama sinema,
Sitamani liishe,
Nitaongeza viungo asili,
Lisipoteze ladha yake,
Penzi lina utamu wake,
Asiyejua ni taka,
Uliza Remeo na Juliet,
Hii letu lipo kudumu kama milima,
Baraka za Mola tunazo,
Ahadi za kitabu takatifu tumetimiza,
Historia ya mapenzi tanaliandika,
Kitahadithiwa mikaka na mikaka,
Hadithi yako litabaki kuwa ajabu ya dunia,
Roho unayo ya utu,
Wafanya upya ujana wangu,
Amani na ustawi nimewai.
© Fely g chronicles
This poem has not been translated into any other language yet.
I would like to translate this poem