Mbona Nchi Twaboromosha? Poem by DEDAN ONYANGO

Mbona Nchi Twaboromosha?

Hodi hodi nabisha, mlango nyie fungueni
Kuna jambo lantatiza, mahasadi pungueni
Swali langu skiza, kama maji ufukweni
Mbona nchi twaboromosha, hasama kila uchao?

Nipe ruhusa niwapashe, harakati zangu mruwa
Kuwajibika sote si kasheshe, bali jambo mrwa
Jami yatupasa tukeshe, kujenga nchi maridhawa
Mbona nchi twaboromosha, hasama kila uchao?

Kukaa kitako ni tatizo, wakati nchi ya chomeka
Kusema hayakuhusu ni wazo bonzo, kaka dada wajibika
Fanya uliwezalo bila tuzo, moyo utaridhika
Mbona nchi twaboromosha, hasama kila uchao?

Kwa miaka na mikaka, nchi yetu twaweka viraka
Katiba twaibaka, ukabila ndio dhihaka
Penda jirani yako kaka, nchi itajengeka
Mbona nchi twaboromosha, hasama kila uchao?

Ni zetu juhudi vijana, kutumika vibaya kupinga
Siasa za fitina achana, zijengazo ndizo nanga
Uchumi tajenga mchana, ufisadi naomba kupinga
Mbona nchi twaboromosha, hasama kila uchao?

Uchafuzi wa mazingira, swala zito nchini
Hewa safi kwa hadhira, afya bora mijini
Uzalendo ni kutengeneza hajira, hasira tupeni
Mbona nchi twaboromosha, hasama kila uchao?

Dini tushike hima, kwa vitendo na maneno
Tusiwe wa kupima, kila wa saa utengano
Tuwe wa busara hima, kila jambo maridhiano
Mbona nchi twaboromosha, hasama kila uchao?

Wakati wangu kesha timia, kuondoka sina budi
Natumai mesikia, na sasa tekeleza juhudi
Bila juhudi taangamia, kuwajibika hatuna budi
Mbona nchi twaboromosha, hasama kila uchao?

Wednesday, August 10, 2016
Topic(s) of this poem: insensitivity
COMMENTS OF THE POEM
READ THIS POEM IN OTHER LANGUAGES
Close
Error Success