Tembea Kenya Poem by priscah Mutswenje

Tembea Kenya

Mebarikiwa Kenya, mrembo wa warembo
Polepole kipenya, uyone yayo mambo
Taona yasomenya, ona ile mitambo
Talii yetu Kenya, pata makuu mambo
Tembea Kenya, Mkenya, ni mimi na wewe

Tavuka yake mito, midogo na mikubwa
Kunayo ilo moto, Poti Ceol livoumbwa
Lipo ziwa la mvuto, Victoria kaumbwa
Bahari kuu la joto, Hindi Yetu tambua
Tembea Kenya, Mkenya, ni mimi na wewe

Milima mesimama, kupokea watalii
Milima Kenya jama, tembelea leo hii
Elgoni waelea, upweke wa asili
Zuru pia Sakina, Longonoti kufadhili
Tembea Kenya, Mkenya, ni mimi na wewe

Wataka kuogelea, njoo kwetu Watamu
Pwani yavutia, joto lake kwa damu
Ukifika tulia, nenda Dunga Kisumu
Satima yangojea, mlima wa makamu
Tembea Kenya, Mkenya, ni mimi na wewe


Tuna wote wanyama, wa mbwembwe na jasiri
Simba hata Ilama, ndovu vifaru ngiri
Taona wakihama, twiga swara fasiri
Mara Tsavo ya zama, mbuga Mboseli nzuri
Tembea Kenya, Mkenya, ni mimi na wewe

Nazo temaduni kumbi, asili nazo nyimbo
Ndizi na kuku shumbi, magharibi ndo jimbo
Samaki nyama tumbi, Nyanza Kitui nyimbo
Pwani kuna ukumbi, tayapata mafumbo
Tembea Kenya, Mkenya, ni mimi na wewe

Miji tele ilonoga, biashara nao ukulima
Wa nane ugongapo, zuru kwalo lolote
Meneo ufikapo, tembea usitoke
Hakuna matata tuliko, Wakenya changamke
Tembea Kenya, Mkenya, ni mimi na wewe

COMMENTS OF THE POEM
READ THIS POEM IN OTHER LANGUAGES
Close
Error Success