Wapo watu na porojo, chupi kutoithamini.
Nalileta kwenu zogo, nijibuni niamini.
chupi thamaniye togo, na ereni sikioni?
Thamani utaijua, siketi wakiivua.
Mwingine alinambia, havai kiso maana.
Akivaa sintojua, Pamoja tutafanana.
Hadhi ya chupi najua, ndo hasa ninapingana.
Thamani utaijua, suruali ikichanwa.
Swali langu la kijinga, majibu mazuri nipe.
Kwa msuli kujifunga, chupi haiwekwi pweke.
Hata wavaao kanga, paso chupi sekeseke.
Thamani utaijua, pale kanga ikilowa.
Tamati nasisitiza, chupi thamaniye kubwa.
Uliza wanolegeza, makalio yanazibwa.
Chupi si ya kubeza, si mtoto si mkubwa.
Thamani utaijua, nguo zote zikiibwa.
This poem has not been translated into any other language yet.
I would like to translate this poem
Umeandika na kuchambua vyema.