Unga Poem by Abdallah Mpogole

Unga

Unga Mwanangu unga,
sijeunga visivyounga,

Unga mpenzi unga, unga twende kukonga.

Unga huo unga wa mahindi wa kusonga.

Unga hizo unga, unga sentensi tunga.

Unga hiyo hoja unga, unga wacha kuvunga.

Unga na nyanya unga, unga mboga ya mchunga.

Unga chakula unga, nani asokula unga.

Unga madawa unga,
yupi anobwia unga.

Unga vipande unga, yupi apenda kutounga.

Unga wa kazini unga, fasidi ndiye tamwagwa unga.

COMMENTS OF THE POEM
READ THIS POEM IN OTHER LANGUAGES
Abdallah Mpogole

Abdallah Mpogole

Iringa, Tanzania
Close
Error Success