LINET SABASTIAN

Silver Star - 3,625 Points (07 JUNE / KENYA)

Mahaba Haba (Swahili Language) - Poem by LINET SABASTIAN

Mahaba tamu, nani hataki kupendwa
Mahaba yako tamu, mbona unipe tu kionjo
Mahaba yako yamenidatisha, kwako sibanduki
Mbona yako mahaba yawe haba kwangu?

Muda wako ungenipa, nikuambie yangu mawazo
Muda wako ungenipa, nikukumbatie nikubusu
Muda wako ungenipa, nikutazame machoni nione lako penzi
Mbona yako mahaba yawe haba kwangu?

Nimekupenda kwa roho yangu yote
Nipe lako tamu penzi si kwa kionjo tu
Nipende kwa vitendo pia si kwa maneno tu
Mbona yako mahaba yawe haba kwangu?

Kwa kweli umenipimia lako penzi, nina njaa na kiu
Kwa kweli umenipimia lako penzi, kama dawa kwa mgonjwa
Kwa kweli umenipimia lako penzi, kama wali wa daku
Mbona yako mahaba yawe haba kwangu?

Fungua wako moyo, unipe yote yako mahaba
Furaha utanipa, kwa kunipa yako mahaba bila kipimo
Furaha utanipa, usiwe bahili wa mahaba
Mbona yako mahaba yawe haba kwangu?

Utajuaje utamu wa mahaba usipopenda?

Topic(s) of this poem: love

Form: Blank Verse


Poet's Notes about The Poem

Utamu wa mahaba

Comments about Mahaba Haba (Swahili Language) by LINET SABASTIAN

 • Rose KananaRose Kanana (10/27/2016 11:33:00 PM)

  Nice to read a Kiswahili poem it makes the message sound deeper. (Report)Reply

  Linet SabastianLinet Sabastian(10/29/2016 10:32:00 AM)

  Thanks Rose. I love your poems.

  0 person liked.
  0 person did not like.
Read all 2 comments »

Rudyard Kipling

IfRead this poem in other languages

This poem has not been translated into any other language yet.

I would like to translate this poem »

word flags


Poem Submitted: Saturday, October 22, 2016

Poem Edited: Friday, November 11, 2016


[Report Error]