Naamba. Poem by Muriungi Martin

Naamba.

Imi nataka niambe, niambe kwa ukabambe,
Sitoamba kwa kithembe, wala kunena kizembe,
Nifikie na mashombe, ngoma yangu na itambe,
Ngoma yangu musikile, amani ndugu amani.

Mara nyingine niimbe, jinsi ya mja wa pombe,
Nikiimbe kisarambe, kote kote kiwakumbe,
Kisababishe uvimbe, uvimbe wa ujumbe,
Wimbo wangu musikile, amani jama amani.

Tena nataka niumbe, niumbe mwema kiumbe,
Tena awe nazo pembe, pembe zile za wajumbe,
Kote kiumbe atambe, nayo mawi asiambe,
Kiumbe wangu muole, Amani kote amani.

Trna niipike pombe, mapishi yangu muimbe,
Nimimine kwa vikombe, tamu hadi chembechembe,
Mpe na wenu vikembe, na makono muyarambe,
Pombe yangu muionje, pombe yangu ya amani.

Kaditamati niombe, kwa Muumba wa viumbe,
Kisa ili tusigombe, hivyo nanyi pia mwombe,
Ili yanyooke mambe, maovu yasitukumbe,
Kwake Mola twelekee, Rahimu tupe amani.

Saturday, July 29, 2017
Topic(s) of this poem: happy
COMMENTS OF THE POEM
READ THIS POEM IN OTHER LANGUAGES
Close
Error Success