Usilie, Vita Ni Karimu. Poem by Muriungi Martin

Usilie, Vita Ni Karimu.

Usilie mwanamwari, kwani vita ni karimu,
Mpenzi wako kisiri, litupa makono gumu,
Mbinguni kuso na heri, imara akajikimu,
Nyamaza dada silie, vita kweli ni karimu.

Ngoma pwewa za majeshi, roho na kiu ya vita,
Kupekecha kiwaashi, lizawa kufa kivita,
Jaha so uthibitishi, juu yao inapita,
Mkuu mungu wa vita, na ugawe wa maiti.

Usilie wewe mwana, kwani vita ni karimu,
Babayo ulimuona, lijikwa' penye mashimu,
Kifua kafura sana, akia hadi kuzimu,
Nyamaza silie mwana, vita kweli ni karimu.

Bendera jeshi kiwaa, kipungu mwe' shungi dha'bu,
Waume lizaliwaa, kufa kipekecha tabu,
Wape wema kunyongea, na kuua ni ajibu,
Na ugani kwa maiti, elfu yao walala.

Roho yako nawe mama, lianga kama kifungo,
Kwa vazi la mwana wima, vulana le vunja ungo,
Kuli e' nina koma, usijipee kinyongo,
Vita kweli ni karimu.

Thursday, July 6, 2017
Topic(s) of this poem: death
COMMENTS OF THE POEM
Muriungi Martin 29 July 2017

welcome

0 0 Reply
Jazib Kamalvi 28 July 2017

Seems nice poetic imagination, Thank you very much,

0 0 Reply
READ THIS POEM IN OTHER LANGUAGES
Muriungi Martin

Muriungi Martin

Meru, Kenya
Close
Error Success