Vita Na Kifo Poem by Muriungi Martin

Vita Na Kifo

Rating: 2.5

Makiwa makiwa mama, umempoteza mwana,
Rajuayo kaditama, mava makazi yafana,
Peke baki kukoroma, maisha tunga kwa kina,
Tukufu vita na kifo, pamwe nyanja za maiti.

Kindakindaki kijana, na kiwi cha kupigana,
Kajitosa pa kufana, na uzoefu hapana,
Miungu ikaitana, kabidi kuandamana,
Uwanja wa hivyo vita, maiti waso idadi.

Mwana pole mwana pole, babayo amekutoka,
Huzuni usiuole, maisha na dhihaka,
Kavitumia vidole, 'tingisha biriti kaka,
Lo! kumbe ndaniye pale, mnazo njiti hakika.

Hivi viroho kwa kweli, vina uroho si haba,
Havijali havibali, kwa kifo vina mahaba,
Kaendea vita mbali, karudi nayo mikoba,
Iliyojaa tikiti, za safari ya angani.

Wednesday, June 21, 2017
Topic(s) of this poem: death
COMMENTS OF THE POEM
READ THIS POEM IN OTHER LANGUAGES
Muriungi Martin

Muriungi Martin

Meru, Kenya
Close
Error Success