KAPCHANGA MARK KWEMOI

Rookie (22.02.1983 / Kitale, Kenya)

Mwanisema Mimi Chongo - Poem by KAPCHANGA MARK KWEMOI

Kukuomba ninaanza, nisadie ewe Mola
Tungo langu linaanza, lisokufanya kulala
Litatoa hata funza, pasi kuzua balaa
Mwanisema mimi chongo, kwa kukosa kunywa tembo

Mwanisema mimi mushamba, sigara hata sivuti
Nasikiliza tu kayamba, Shakiraa simupati
Lahaja zangu eti kwamba, sineni po’ wala fiti
Kwa kukosa kunywa tembo, mwanisema mimi chongo

Uraibu wenu pombe, mijini usiku mupo
Mwala miraa na tembe, mwanyea pale mulipo
Mwameesha ndefu pembe, mwanisema kuwa popo
Nyama zenu zangu sumu, binadamu wote si sawa

Warembo popote nao, cheteni hata skulini
Suruali ndefu ndio, ya kufika mavumbini
Usoni mwaweka vyoo, aso navyo yeye duni
Uraibu wetu nini, wendani nawauliza

Wendani nawauliza, munijibu tafadhali
Mwaniweka ujuza, napoteza yangu hali
Ni muhali kuwaguza, lakini vema kukili
Utata wenu starehe, mubadili enyi ndugu

Sigara sio silaha, marijuana yauwa
Tapoteza yako siha, hatimaye kupagawa
Tusijitie ujuha, kuna wema wanojuwa
Kanisani vema twende, mola atupe baraka

Kaditama beti saba, niloudhi samahani
Tuwape akina baba, heshima tusiwatani
Bidii isiwe haba, muhimu sana chuoni
Mwanisema mimi chongo, kengeza kwao warembo


Comments about Mwanisema Mimi Chongo by KAPCHANGA MARK KWEMOI

There is no comment submitted by members..Read this poem in other languages

This poem has not been translated into any other language yet.

I would like to translate this poem »

word flags

What do you think this poem is about?Poem Submitted: Wednesday, April 16, 2008[Report Error]