KAPCHANGA MARK KWEMOI

Rookie (22.02.1983 / Kitale, Kenya)

Tuepuke Vurumai - Poem by KAPCHANGA MARK KWEMOI

Nalitunga tungo hili, pasi kiwewe moyoni
Maulana nipe tuli, nisije nena utani
Nitege kitendawili, inayokera amani
Uchaguzi ndio huu, tuwepuke vurumayi.

Fujo taleta hasara, tusoweza kuzikimu
Tasababisha fukara, wengine tawa wazimu
Tuwaepuke majura, wanoleta uhasimu
Tuwepuke zogo zogo, uchaguzi waja punde.

Tusiwape masikio, wanohubiri ghasia
Tatuletea kilio, isoweza kupungua
Marekani wana wao, hawajali mukilia
Mizozo tuepukane, maovuye kochokocho.

Watasema yule mbaya, mutoe shingo alale
Muwawekee faya, damu yao ndo kilele
Kabila hiyo ni mbaya, wasiende katu mbele
Maovuye kochokocho, vurumai tuepukane.

Sote siye tu mandugu, kikuyu jaluo moja
Tusiwe adui sugu, damu isije kavuja
Aliyetuumba Mungu, kanisani twende kuja
Ukabila jambo baya, husababisha wadui.

Tungo hili tulisome, tupendane ewe kaka
Shuleni twende tusome, uhasama kuepuka
Kanisa isiwe mahame, vita inapolipuka
Sisi sote tuko sawa, wame waume ni sawa.

Ewe Mola tudekezi, uchaguzi wa amani
Wasadie hata wezi, waepushe wanozini
Bora wawe viongozi, wanopenda upinzani
Tupigapo kura hii, tupuuze uchochezi


Comments about Tuepuke Vurumai by KAPCHANGA MARK KWEMOI

There is no comment submitted by members..Read this poem in other languages

This poem has not been translated into any other language yet.

I would like to translate this poem »

word flags

What do you think this poem is about?Poem Submitted: Wednesday, April 16, 2008[Report Error]