KAPCHANGA MARK KWEMOI

Rookie (22.02.1983 / Kitale, Kenya)

Huba Ja Ukimwi - Poem by KAPCHANGA MARK KWEMOI

Ninalia kwa ukiwa, nifanyeje nimeshindwa
Gani huba lake dawa, hili sijapata ‘lewa
Muumba hana usawa, naishi kama mfiwa
Kupenda usikopendwa, ni simanzi na ukimwa

Kimanzi ndivyo hitwa, nami humwita kisurwa
Ubongo metawaliwa, na viroja na makubwa
Nielezeje makiwa, machozi nimeishiwa
Kupenda usikopendwa, ni simanzi na ukimwa

Maneno ya chengi kinywa, mekosa kuyaelewa
Ombi langu kataliwa, ninaishi kwa ukiwa
Huba moyo ni jangwa, sura tamu kama chungwa
Kupenda usikopendwa, ni simanzi na ukimwa

Kyumbe kama malaika, adimu kupatikana
Vibaya kutamanika, changanyiwa napomwona
Akili kunichanika, mawazo kunijazana
Kupenda usikopendwa, ni simanzi na ukimwa

Ni kimwana liyeumbwa, kamilika bila pewa
Ulimbwende chekwachekwa, hurulaini husemwa
Nikionapo kifuwa, kwa mola upinga duwa
Kupenda usikopendwa, ni simanzi na ukiwa

Hani so mrefu sana, wala so mfupi sana
Hani so mnene sana, wala so mwembamba sana
Hano so mweusi sana, wala so mweupe sana
Kupenda usikopendwa, ni simanzi na ukiwa

Meno sawa na maziwa, macho yake ya gololi
Nywele zilizolanishwa, kama nyuzi za harili
Mashavu yaloumuwa, midomo ja pilipili
Kupenda usikopendwa, ni simanzi na ukiwa

Si mpayukaji ovyo, aidha si mnyamavu
Si mcheka ovyo ovyo, mithili ya miumbavu
Ni mweledi wasemayo, na siyo maneno kavu
Kupenda usikopendwa, ni simanzi na ukiwa

Meli kalia damu, kanikata aslani
Kuishi kukawa vigumu, anikaa akilini
Namhisi yangu damu, habanduki mtimani
Kupenda usikopendwa, ni simanzi na ukiwa

Wangu hani nozunika, daima nakulilia
Langu huba kuloweka, fanaka tumainia
Nilale na kuamka, kwone wangu chapukia
Nakupenda sipendeke, aushi naomboleza.


Comments about Huba Ja Ukimwi by KAPCHANGA MARK KWEMOI

There is no comment submitted by members..Read this poem in other languages

This poem has not been translated into any other language yet.

I would like to translate this poem »

word flags

What do you think this poem is about?Poem Submitted: Wednesday, April 16, 2008[Report Error]