KAPCHANGA MARK KWEMOI

Rookie (22.02.1983 / Kitale, Kenya)

Uzembe Chombo Duni - Poem by KAPCHANGA MARK KWEMOI

Washairi ndugu zangu, nawambie msikie
Wendani sina uchungu, meona niwambie
Bidii yangu ulimwengu, darahima menipa mie

Raha zangu ziko wapi, mbona nyinyi hamuzioni?
Nyinyi mko vipi, kwa bongo lenu kichwani?
Wenye inda mko wapi, hamtanidhuru mwilini

Hata hapa duniani, ili mtu angurume
Kwa mambo yote ya shani, mimi naepuka ukame
Mi najihami kazini, ili uzembe ukome

Maisha kama sunami, ni halambe yenye nguvu
Bila Akili kichwani, utaitwa mpumbavu
Ufanye kazi duniani, usikubali uvivu

Mahitaji sasa mengi, elimu ina faida
Maisha bila msingi, haitaleta msaada
Mariko mimi serehangi, najipunguzia shida

Hatimaye si utani, mimi navunja ngome
Hautatoka maruhani, ni wewe mwenye uime
Usipokuwa rubani, utaitwa gume gume


Comments about Uzembe Chombo Duni by KAPCHANGA MARK KWEMOI

There is no comment submitted by members..Read this poem in other languages

This poem has not been translated into any other language yet.

I would like to translate this poem »

word flags

What do you think this poem is about?Poem Submitted: Wednesday, April 16, 2008

Poem Edited: Wednesday, April 16, 2008


[Report Error]